Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wa Shirika la NORBERT & FRIENDS MISSIONS/OPERATIONAL INTERNATIONAL wanayo furaha kuutaarifu Umma juu ya ujio wa Madaktari bingwa, Wauguzi na wataalamu wa usingizi kutoka Nchini Marekani kwa ajili ya kambi maalumu ya kutoa huduma ya Upasuaji wa Kibingwa kwa Wananchi wote wa Wilaya ya Tanganyika na Mkoa wa Katavi kwa Ujumla
Kambi hiyo ya Madaktari bingwa 18 kutoka Marekani itaanza tarehe 06/04/2024 hadi tarehe 13/4/2024 katika Hospitali ya wilaya ya Tanganyika.
Moja ya huduma zitakazotokewa ni pamoja na
1. Ngiri/Hermia
2. Goita
3. Uvimbe kichwani na Shingoni
4. Midomo Sungura
5. Uvimbe kwenye mfumo WA chakula
6. Makovu kuvu
7. Uvimbe kwenye ngozi
NB: Huduma za Upasuaji zitafanyika Bila Malipo yoyote isipokuwa Uchangiaji Mdogo wa Dawa na Vipimo tu.
Kwa maelezo zaidi wasilina na Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Alex Mrema 0759 - 916 - 262
WOTE MNAKARIBISHWA.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.