Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika umefanya kikao muhimu katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Bodi ya Ajira.
Lengo kuu la kikao hiki lilikuwa kujadili na kuthibitisha upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma waliotimiza vigezo vya kiutumishi. Hii ni hatua muhimu katika kuthamini mchango wa watumishi na kuimarisha ari ya utendaji kazi serikalini.
Kikao kimeidhinisha rasmi majina ya watumishi wanaopandishwa vyeo, na taratibu za kuwatangazia na kuwapatia barua za uthibitisho zitaanza mara moja kupitia Idara ya Utumishi.
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika itaendelea kusimamia misingi ya haki, uwazi na ufanisi katika usimamizi wa rasilimali watu.
“Motisha kwa Watumishi ni msingi wa huduma bora kwa wananchi.”
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.