Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilayani Tanganyika mkoani Katavi, Mh. Yasin Kiberiti amewataka wananchi wilayani humo kuachana na imani potofu na vitendo vya kishirikina vinavyojihusisha na kutoa watu uchawi maarufu kama Kamchape na Lambalamba,
Mheshimiwa Kiberiti ameyasema hayo jana wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi wilayani humo yenye lengo la kukagua miradi, kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao,
Katika ziara hiyo, Mh. Kiberiti aliambatana na waaalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika ili kumsaidia kutolea majibu changamoto mbalimbali zinazoibuliwa na kulalamikiwa na wananchi.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.