Waheshimiwa Madiwani, Watumishi wa Umma na Viongozi wa Halmashauri za Wilaya ya Momba ya Mkoani Songwe na Makete ya Mkoani Njombe wametakiwa kuwa na mshikamano kama wanataka kufanikiwa kutekeleza biashara ya Kaboni kwenye maeneo yao,
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mheshimiwa Onesmo Buswelu alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa halmashauri hizo ambazo zimetembelea wilayani Tanganyika kwa lengo la kujifunza kwa ufasaha namna sahihi ya kutekeleza biashara hiyo,
Mheshimiwa Buswelu amewasisitiza wageni hao kuwa, Biashara ya Kaboni ni biashara nzuri yenye fedha za kutosha lakini inahitaji umoja, bidii na mshikamano kutoka kwa makundi yote katika jamii,
"Kama mnataka kufanikiwa kabisa katika biashara hii basi ni lazima muunganishe nguvu katika makundi yote ndani ya jamii zenu muwe kitu kimoja ndipo mtaweza kuona matunda ya biashara ya Kaboni" amesema DC Buswelu,
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Hamad Mapengo amesema kuwa ni jukumu la viongozi wote kuanzia ngazi ya serikali, halmashauri, chama tawala na makundi yote katika jamii kuwa kitu kimoja ili kuweza kufanikisha biashara ya Kaboni,
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw. Shaban Juma amesema kuwa miongoni mwa chanzo cha mapato kinachosaidia kusukuma gurudumu la maendeleo wilayani Tanganyika ni pamoja na biashara ya Kaboni mpaka sasa miradi mbalimbali ya afya, elimu na kijamii imeendelea kutekelezwa wilayani hapa kutokana na mapato ya biashara hiyo,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeendelea kujizoea umaarufu ndani na nje ya nchi kwa kufanikiwa kutekeleza vyema biashara ya Kaboni na kuwezesha kuingiza mapato ya zaidi ya shilingi Bilioni 22 tangu kuanza kwa biashara hiyo mpaka sasa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.