Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mh. Shaban Juma ametembelea maeneo ya Ikola na Karema kwa lengo la kujionea madhara yaliyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na upepo mkali uliopelekea maji ya ziwa Tanganyika kukimbilia kwenye makazi ya wananchi,
Mheshimiwa Shaban Juma aliongozana na Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Mrindoko ambapo pia alipokea maagizo kutoka kwa Mkuu wa mkoa huyo ya kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wanapatiwa huduma za muhimu zikiwemo za afya na makazi,
Vijiji vya Ikola na Karema vilikumbwa na kadhia hiyo hivi karibuni ambapo kaya zaidi ya 200 zimeathiriwa moja kwa moja.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.