Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh. Onesmo Buswelu leo amekagua ujenzi wa dharura wa barabara ya Mkokwa - Mnyagala na kuagiza ujenzi wake uende haraka ili wananchi waweze kuitumia barabara hiyo kwa shughuli zao mbalimbali,
Mheshimiwa Buswelu ametoa maagizo hayo leo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo na kukuta mafundi wakiendelea na ujenzi kama kawaida,
"Naomba muongeze kasi ya ujenzi wa hii barabara ili wananchi hawa wa maeneo haya wanaotumia hii barabara waendelee na shughuli zao bila kikwazo chochote" alisema Mh. Buswelu
Ujenzi wa barabara hiyo utahusisha uwepo wa makalvati 9, madaraja ya kati 2 sambamba na uwekaji wa tuta na changarawe katika maeneo yote korofi zaidi ya kilomita 2.
Mpaka kukamilika kwake, ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 200, fedha kutoka serikali kuu.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.